in , , , , , , ,

YANGA Watamba Tuzo za Februari Ligi Kuu ya NBC 2024/25

DUBE MCHEZAJI BORA FEBRUARI LIGI KUU YA NBC 

YANGA Watamba Tuzo za Februari Ligi Kuu ya NBC 2024/25

MSHAMBULIAJI
wa timu ya Young Africans (Yanga) ya Dar es Salaam, Prince Dube,
amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya NBC
msimu wa mwaka 2024/25, huku Miloud Hamdi pia wa Yanga akichaguliwa
Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo.

YANGA SC Watamba Tuzo za Februari Ligi Kuu ya NBC 2024/25
Prince Dube

Dube
alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akiwashinda Aziz Ki wa Yanga
na Selemani Bwenzi wa KenGold, alioingia nao fainali katika mchakato wa
Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).
READ ALSO:

Mchezaji
huyo alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo saba ambayo
Yanga ilicheza mwezi huo na kufunga mabao matano na kuhusika na mengine
matano kwa dakika 562 alizocheza. Yanga ilishinda michezo sita na kutoka
sare mmoja.

Kwa upande wa Hamdi aliyeingia fainali katika
mchakato huo na Fadlu Davids wa Simba na Fred Minziro wa Pamba Jiji,
aliiongoza Yanga kushinda michezo minne na sare moja, ambapo kwa mwezi
huo Yanga ilicheza michezo saba.

Hamdi aliiongoza Yanga
ilipotoka suluhu na JKT Tanzania, kisha ikazifunga KMC mabao 1-6,
Singida Black Stars (2-1), Mashujaa (0-5) na Pamba Jiji (0-3). Mechi
nyingine ambazo Yanga ilishinda mwezi huo lakini haikuwa chini ya Hamdi
ni dhidi ya KenGold (6-1) na dhidi ya Kagera Sugar (4-0).

Pia
Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo
uliopo Dar es Salaam, Ashraf Omar, kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi
Februari kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya
michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

logoblog





JOIN US ON TELEGRAM
Get Notifications Faster by:

NBC Premier League Statistics 2024/25: Top Scorers, Top Assist and Top Clean Sheets

KYARUZI, SIMCHIMBA Wang’ara Tuzo za NBC Championship 2024/2025