in , , , , ,

KYARUZI, SIMCHIMBA Wang’ara Tuzo za NBC Championship 2024/2025

KYARUZI, SIMCHIMBA Wang’ara Tuzo za NBC Championship 2024/25
Tuzo za NBC Championship 2024/25

KYARUZI,SIMCHIMBA WANGARA TUZO ZA NBC CHAMPIONSHIP

KYARUZI, SIMCHIMBA Wang’ara Tuzo za NBC Championship 2024/25

BEKI
wa Mtibwa Sugar Erick Kyaruzi amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi
Januari wa Ligi ya NBC Championship 2024/25, huku Awadh Juma wa Mtibwa
Sugar akichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo.

Kyaruzi aliyeingia
fainali katika mchakato huo na Raizin Hafidh wa Mtibwa Sugar na Boniface
Maganga wa Mbeya Kwanza, alionesha kiwango chenye mwendelezo katika
safu ya ulinzi, huku pia akisaidia timu yake kwa kufunga mabao mawili
katika dakika 270 za michezo mitatu aliyotumika.

Kwa upande wa
Awadh aliyeingia fainali na Zuberi Katwila wa Bigman na Emmanuel Massawe
wa Mbeya Kwanza, aliiongoza timu yake kupata ushindi katika michezo
yote mitatu iliyocheza ikivuna pointi tisa na kuendelea kuongoza ligi
hiyo.
READ ALSO:

Pia
kamati imemchagua Andrew Simchimba wa Geita Gold kuwa Mchezaji Bora wa
Mwezi Februari wa Ligi ya NBC Championship 2024/25, huku Mohamed Muya
pia wa Geita Gold akichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo.

Simchimba
aliyeingia fainali katika mchakato huo na Oscar Tarimo wa Mbeya Kwanza
na Mwisho Yangson wa Polisi Tanzania alionesha kiwango chenye mwendelezo
ikiwa ni pamoja na kufunga mabao manne katika michezo mitatu kwa dakika
253 alizocheza.

Kwa upande wa Muya aliyeingia fainali na Zuberi
Katwila wa Bigman na Juma Hussein wa Stand United, aliiongoza timu yake
kushinda michezo minne kati ya mitano iliyocheza mwezi huo.

logoblog





JOIN US ON TELEGRAM
Get Notifications Faster by:

YANGA Watamba Tuzo za Februari Ligi Kuu ya NBC 2024/25

2 New Various Jobs at IUCN Tanzania March 2025